KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma amekugua miradi minne na kuzindua miradi minne yenye thamani ya shilingi Milioni 382.3 katika Halmashauri ya Madaba Mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika Mbio hizo amepongeza usimamizi wa miradi hiyo na kuwataka viongozi wa Halmashauri ya Madaba kuendelea kusimamia miradi hiyo ya Serikali.
Ndugu Geraruma amekagua mradi wa kikundi cha Maarifa Mtyangimbole, mradi wa Lishe Zahanati ya Magingo, mradi wa ugawaji vyandarua Zahanati ya Magingo pamoja na ugawaji wa pikipiki kikundi cha Umoja wa Madereva Bodabada Madaba.
‘’Ndugu zangu wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano hakikisha unazingatia sana elimu kuhusiana na mapambano dhidi ya Malaria kwa kutumia vyandarua vyenye dawa, kuhudhuria clinic pamoja na matumizi bora ya Lishe’’, amesisitiza Geraruma.
Pia amezindua madarasa mawili shule ya sekondari Lipupuma, Klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Magingo, madarasa matatu na ofisi shule ya sekondari Mahanje pamoja na Anwani za Makazi na Postikodi.
‘’Pongezi kubwa ziende kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba na pongezi hizo ni kwasababu ya marejesho ya fedha za maendeleo ya vijana alizozirejesha kwa wakati’’, amesema Geraruma.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololet Mgema amemshukuru kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa kuukimbiza Mwenge salama na ameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa.
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Madaba ulipokelewa tar 13/04/2022 na ulikimbizwa jumla ya kilomita 247 na umepita katika vijiji 15, Kata sita na Tarafa moja.
Imeandikwa na Bahati Nyoni
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Aprili 19 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.