Mwenge wa Uhuru 2024 umeikubali miradi yote yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni moja iliyoipitia katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Akizungumza kwenye makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Halmashauri ya wilaya ya Songea na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga,Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Kisare Makori amesema Mwenge huo katika Halmashauri hiyo umekimbizwa jumla ya kilometa 110.9 na kutembelea miradi sita yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1.
Akitoa taarifa ya ufunguzi wa mradi wa kituo cha Afya Litumbandyosi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Rwiza amesema hadi sasa Zaidi ya shilingi milioni 824 zimetumika kujenga kituo hicho ambacho kinahudumia wakazi 11,506 wa Kata ya Litumbandyosi.
Ametaja lengo la kujenga kituo hicho ni kusogeza huduma za afya kwa wananchi ili kupunguza gharama za matibabu kwa wakazi wa Kata hiyo yenye vijiji vinne vya Mabuni,Luhagara,Kingoli na Litumbandyosi.
Mradi mwingine uliopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni shamba la miti ya mitiki lililopo katika Kijiji cha Mabuni lenye jumla ya miti 2,692 linalomilikiwa na Festo Mhagama.
Mwenge wa uhuru pia umetembelea chanzo cha chemchem ya Mto Askofu uliopo katika Kijiji cha Paradiso Kata ya Ruanda ambapo Chemchem hiyo ina uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita 16,000 kwa siku na ipo katika hifadhi ya msitu wa Kijiji cha Paradiso chenye wakazi wapatao 2,766.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godrey Mnzava ameridhia kuzindua mradi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari Ruanda ambayo yamegharimu Zaidi ya shilingi milioni 48.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pia umekagua kikundi cha wanawake kinachoitwa Umoja wa Wanawake Mbalawala ambacho kinaendesha mradi wa utengenezaji na uuzaji wa nishati ya makaa ya mawe ya kupikia ambapo jumla ya shilingi milioni 130 zimetumika kutekeleza mradi huo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.