Mwenyekiti wa UWT taifa Mary Chatanda amewasifu viongozi wa wilaya ya Namtumbo Kwa kusimamia vyema fedha za miradi inayotekelezwa Katika wilaya ya Namtumbo .
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa sekondari ya wasichana iliyopewa jina La Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Mradi wa ujenzi wa Jengo la Mama ngojea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo alisema anawasifu viongozi wa wilaya ya Namtumbo Kwa kusimamia vyema fedha za miradi Kwa kuwa na majengo Bora yanayoakisi matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa.
"Nimefurahishwa Sana na usimamizi wa fedha za miradi inayotekelezwa Katika wilaya ya Namtumbo ,miradi mizuri inapendeza inayolingana na gharama halisi ya fedha iliyotolewa na Serikali alisema Chatanda.
Pamoja na hayo Mwenyekiti waUWT. taifa aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha mabweni ya Sekondari ya Dkt.Samia Suluhu Hassan yanakuwa na maji ya uhakika ,umeme wa uhakika muda wote Ili Shule hiyo iendane a hadhi ya Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliwataka walimu watakaofundisha shule hiyo kuhakikisha wanafundisha Kwa kujituma Ili wanafunzi waweze kufanya vizuri huku akiwaahidi walimu pikipiki Ili waweze kuwahi kazini , kutokana na walimu kukosa Nyumba za kuishi jirani na maeneo ya shule hiyo
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa pamoja na kumshukuru Mwenyekiti wa UWT taifa Kwa kujionea mwenyewe kuhusu utekelezaji wa miradi alimwomba kuzifikisha salamu za shukrani za wananchi wa wilaya ya Namtumbo Kwa Mheshimiwa Rais ,Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwapatia fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo .
Mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Robert Magesa alimwambia Mwenyekiti huyo kuwa ujenzi wa miradi mbalimbali unaendelea vizuri wilayani humo Kwa kuzingatia miongozo iliyopo na uwepo wa usimamizi wa karibu wa viongozi Ili miradi hiyo ikidhi viwango vilivyowekwa na Serikali kulingana na fedha tolewa alisema Magesa.
Mwenyekiti wa UWT taifa Mary Chatanda alikagua mradi wa ujenzi wa sekondari ya Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na jengo la mama ngojea na kusema kuwa anawasifu viongozi wa wilaya ya Namtumbo Kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu hiyo na kudai kuwa ameridhika na ubora na uzuri wa majengo hayo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.