Naibu Kamishna wa Skauti Taifa, Bi. Amina Clement, amefanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo na kukutana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Ngollo Malenya.
Ziara hiyo imelenga kujadiliana juu ya mbinu za kuwahamasisha vijana kuhusu ukakamavu, uzalendo, na kujitambua.
Katika mazungumzo yao, Bi. Amina alisisitiza umuhimu wa kuwajengea vijana msingi bora wa maadili, nidhamu, na kujituma ili wawe viongozi bora wa baadaye.
Pia, alieleza kuwa juhudi hizi zinaenda sanjari na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwaletea maendeleo wananchi, hususan vijana.
Alifafanua dhamira ya Skauti Taifa ya kushirikiana na viongozi wa serikali ili kuhakikisha vijana wanapata elimu ya ukakamavu na uongozi katika ngazi zote.
Alisisitiza umuhimu wa malezi bora kwa vijana kuwa ndiyo msingi wa taifa imara na lenye viongozi wenye maadili.
Kwa upande wake, Mhe. Malenya alisema ofisi yake ipo tayari kushirikiana na Skauti Taifa kuwa ili kufanikisha malengo hayo. Pia, alipongeza alimpongeza Kamishina huyo kwa kuwaandaa vijana kwa maisha ya baadae .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.