Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde, leo Tarehe 18.12.2021 amefanya Ziara ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa madarasa yanayoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Akiwa Wilayani hapa ametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari Limbo, iliyopo Kata ya Kilosa na Sekondari ya Mbamba bay iliyopo Mbamba bay Wilayani hapa
Mara baada ya Kukagua miradi hiyo amesema Halmashauri ya Nyasa inatakiwa kuongeza kasi ya ujenzi kwa kujenga usiku na mchana na mpaka kufikia 31 desemba mwaka huu madarasa yote yawe yamekamilika, kwa kuwa bado ipo kwenye muda wa utekelezaji wa miradi hii kama ilivyopangwa na Serikali.
Ameongeza kuwa Serikali imetoa fedha hizi ili kutatua changamoto ya miundombinu, hasa madarasa katika shule za wilaya ya Nyasa hivyo tunakila sababu ya kutekeleza Miradi hii kwa haraka na ubora wa Hali ya juu.
“Nimetembelea na kuona miradi miwili ambayo ni sampuli ya miradi mingine nimeona mnatakiwa kuongeza kasi ya ujenzi ili ifikapo 31 mwezi Desemba iwe imekamilika kwa asilimia 100 .
Awali akitoa Taarifa ya Miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas amesema ifikapo Desemba 25 mwaka huu miradi yote itakuwa imekamilika kwa kuwa miradi yote ipo kwenye hatua ya ukamilishaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.