Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma limepokea Mapendekezo ya kuanzisha vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani.
Diwani wa kata ya Mkongo Mheshimiwa Daniel Nyambo alisema Mapendekezo hayo ni mazuri lakini akaomba madiwani wapate muda wa kupitia vyanzo hivyo na baraza lijalo waweze Kutoa maamuzi.
Mheshimiwa Lukas Njogopa ni Diwani wa kata ya Rwinga alisema kuwa ni vyema waheshimiwa madiwani wakapitie vyanzo hivyo vya mapato Ili katika Baraza lijalo waje na maamuzi mazuri
Katibu wa Kamati ya Mapato ambaye ni Afisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Musa Mumina katika taarifa amevitaja vyanzo vipya vya mapato vinavyopendekezwa ni pamoja na ujenzi wa vibanda vya biashara,ujenzi wa karakana ya magari na mitambo,mashine ya kufuatilia tofali za saruji.,kiwanda Cha maji ya chupa na ujenzi wa shule ya Sekondari.
Vyanzo vingine amevitaja kuwa ni ununuzi wa mashine ya kuchakata kokoto,ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao,ujenzi wa stendi ndogondogo kwenye ngazi ya kata na vijiji pamoja na kituo Cha kuuza mafuta(Petrol station)
Mapendekezo ya vyanzo vipya vya mapato katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo yatatolewa katika baraza la madiwani la robo yapili linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.