• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NATANGAZA vita endelevu na wanaokata miti kwenye hifadhi-RC Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: January 13th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  amesema kuanzia sasa anatangaza vita endelevu  na watu wote wanaokata miti kwenye misitu na wanaoharibu vyanzo vya maji.

Ametangaza vita hiyo kwa nyakati tofauti  wakati anazindua upandaji wa miti shuleni katika wilaya za Mbinga na Nyasa.

RC Thomas amewaagiza wakuu wote wa wilaya, wakurugenzi, maafisa tarafa,kata na vijiji kusimamia sheria mama ya mazingira ili kulinda misitu na vyanzo vya maji.

“Wilaya ya Mbinga inaongoza kwa kuharibu misitu na kuacha milima ikiwa vipara,ninyi kila mahali mnapoona miti mnatembea na shoka na kuteketeza miti,muone aibu mna ugomvi gani na miti’’,alihoji RC Thomas.

Amesisitiza kuwa anaanzisha ugomvi na wakata miti na wanaoharibu vyanzo vya maji kutokana na kufanya shughuli za kibinadamu hadi ndani ya vyanzo vya maji.

Ameongeza kuwa amebaini maeneo mengi  yenye hifadhi za misitu zikiwemo hifadhi ambazo zipo chini ya Wakala wa Misitu Tanzania TFS na kwenye vyanzo vya maji na maeneo ya misitu ya vijiji yanavamiwa na kukatwa miti hivyo amewaagiza wadau wote wa mazingira kuyalinda maeneo hayo kikamilifu.

Ameagiza miti yote inayopandwa itunzwe ili iweze kukua na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yaliyoanza kuleta athari katika baadhi ya maeneo ikiwemo mito na vyanzo vya maji kukauka na kukosa mvua za uhakika.

Amesema upandaji miti na kulinda vyanzo vya maji iwe ni kampeni ya kudumu,ambapo amesisitiza kuwa ameamua kuzindua kampeni ya kupanda miti katika shule ili kujenga tabia ya kupenda kupanda miti kwa watoto kuanzia shule za msingi, sekondari,vyuo vikuu hadi wanapokuwa watu wazima.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza TFS kuhakikisha kila shule mkoani Ruvuma inapewa miche ya miti ya kutosha kwa ajili ya kupanda kwenye mazingira yao.

Awali akitoa taarifa ya upandaji miti katika Wilaya ya Mbinga katika kipindi cha mwaka 2022/2023,Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo amesema wilaya hiyo ina misitu mitano ya hifadhi ambayo ni Namswea, Liwiliktesa, Kigonsera, Amanimakoro na Lupembe.

Mangosongo amesema wilaya hiyo pia ina mashamba ya miti ya kupandwa ambayo ni Mbambi, Ugano, Likopesi, Ndengu,Mpapa,Lubela,Mahenge na Mbuji na kwamba misitu hiyio inasimamiwa na Halmashauri ya Wilaya na Serikali Kuu.

“Uzinduzi wa upandaji miti katika shule,ni kielelezo cha upandaji miti katika wilaya ya Mbinga ambao unaenda sanjari na ugawaji wa miche ya miti kibiashara  iliyooteshwa na  TFS’’,alisema.

Amesema TFS katika wilaya ya Mbinga imezalisha miche ya aina mbalimbali 208,650 kati yao hiyo misindano 67,120,misaji 9,650,mibolea 13,020, mikaratusi 121,838,miembe 300,michungwa 200, parachichi 500,mikangazi 800 na misedelela 300.

Katika wiki maalum ya upandaji miti mkoani Ruvuma iliyoanzia Januari Mosi hadi 7,2023 jumla ya  miche ya miti ya asili 1,100,000  iliyotolewa na TFS imepandwa.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 13,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.