WAKAZI wa vijiji viwili vya Misechela na Liwanga kaya Misechela wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanakwenda kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya serikali kutoa zaidi ya shilingi bilioni tatu ili kutekeleza mradi wa maji utakaowanufaisha wakazi zaidi ya 9,050 wa vijiji hivyo.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Tunduru Mhandisi Maua Mgallah amesema ,ujenzi wa mradi huo umeanza tangu Novemba 2023 na unatarajia kukamilika ifikapo Novemba 2024 .
Amezitaja azi zilizopangwa kufanyika katika mradi huo ni ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 300,000,ujenzi wa tenki la chini la lita 75,000,ujenzi wa banio,uchimbaji wa mitaro na kulaza mabomba umbali wa mita 24,890 na kujenga vituo 28 vya kuchotea maji.
Diwani wa kata ya Misechela Zuber Binamu,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizowezesha kuanza kwa ujenzi wa mradi huo ambao utakapokamilika utamaliza kabisa changamoto ya maji katika vijiji vya Misechela na Liwanga.
Amesema ,kwa muda mrefu wananchi hasa wanawake wa vijiji hivyo wanateseka kwa kuamka usiku wa manane na kutembea umbali mrefu hadi mto Ruvuma kwenda kuchota maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.