Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Mazao ya Kilimo cha Songea Namtumbo (SONAMCU), Bw. Juma Mwanga amesema mkoa wa Ruvuma ni mkoa wa pekee nchini unaolima aina tatu za tumbaku
Hayo ameyasema katika ufunguzi wa Ghala chama cha ushirika cha NAMITILI AMCO katika tarafa ya Nakapanya wiliyani Tunduru alisema kwa kuzingatia maagizo ya Serikali vyama vya ushirika visitegemee zao la aina moja tumekuja kuungana na nyinyi ili kuhakikisha mnalima mazao mengine
”Ndugu zangu tumbaku tunayo ileta sio hile ya miaka iliyopita Mkoa wa Ruvuma ndio mkoa pekee unaolima tumbaku za aina tatu ukilinganisha na maeneo mengine mkoa wa Ruvuma tunalima tumbaku ya mvuke ,moshi pamoja naya hewa”amesema Mwanga
Mwanga alisema katika Wilaya ya Tunduru wamehimiza wakulima walime tumbaku ya hewa ambayo inaendena na hali ya hewa ya wilaya hiyo kwani kilo moja inagharimu shilingi elfu 4,800 hivyo tulime kwa kuinua uchumi wetu
alieleza kwamba chama chao kimeongeza hamasa zaidi kwa vyama vya msingi ili wakulima walime tumbaku na waweze kukidhi mahitaji ya soko
“SONAMCU Tulikuwa na wanachama 46 lakini katika msimu wa 2022/2023 tumehamasisha vyama vya msingi 62 na vyote vimeahidi kulima zao la tumbaku.”amsema Mwanga
Pia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku ya mbolea ili kumpunguzia mzigo mkulima alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa ruzuku ya mbolea kwani bei ya mfuko mmoja ni sh. 70,000 ukienda popote pale hapa wilayani
Vile vile aliomba Serikali ifanye jitihada za makusudi kwa kuajiri maafisa ugani kwenye halmashauri ili wawasaidie wakulima walioko vijijini. Pia aliomba Serikali isaidie kupatikana kwa mikataba (bilateral agreements) baina yake na nchi za Tunisia, Misri na Algeria ambako kuna wanunuzi wakubwa wa tumbaku ya moshi inayozalishwa wilayani humo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.