SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imetoa kiasi cha shilingi milioni 650 kwa ajili yta kutekeleza ujenzi wa nyumba nane za watumishi.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Grace Quentin amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 300 zinatumika kujenga nyumba ya Mkurugenzi nye ghorofa moja na milioni 350 zinatumika kujenga nyumba saba za wakuu wa Idara.
Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Aprili mwaka huu hadi sasa umefikia asilimia 70 na unatarajia kukamilika Juni mwaka huu.Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mkurugenzi huyo amesema anamshukuru Rais kwa kutao mabiilioni ya fedha ambayo yanaendelea kutumika kutekeleza miradi ya majengo ya utawala na afya na kwamba Halmashauri imejipanga kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kulingana na mkataba.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameupongeza uongozi wa Halamshauri hiyo kwa kutekeleza miradi yote inayopewa fedha na serikali kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.