MKUU wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo amezindua kampeni ya Bonge la mpango Kanda ya kusini inayotekelezwa na Benki ya NMB.
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo uliofanyika ndani ya stendi ya mabasi mjini Mbinga, Mwakilishi wa Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Roman Degeleki amesema katika kampeni hiyo zaidi ya shilingi milioni 260 zitatolewa kama zawadi kwa washindi zaidi ya 100.
“kampeni hii itaendeshwa ndani ya wiki 12 kila wiki washindi 12 watapokea shilingi laki moja kila mmoja.mshindi mmoja atajipatia shilingi 200,000 na mshindi mmoja atajishindia pikipiki”,alisema Degeleki.
Ameongeza kuwa katika kampeni hiyo washindi watano watajinyakulia shilingi milioni moja kila Mwisho wa mwezi.
Hata hivyo amesema katika kuhitimisha kampeni hiyo,washindi 11 watajishindia pikipiki,washindi watano watajishindia bajaj na wengine saba watajishindia vifaa vya kieletroniki.
Machi 29 mwaka huu benki ya NMB ilizindua kampeni maalum yenye makusudi ya kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha wa kujiwekea akiba kwa watanzania ambapo hadi sasa wateja wa NMB zaidi ya 70 wamejinyakulia zawadi mbalimbali.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo ametoa rai kwa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa kufungua akaunti katika benki ya NMB.
“Ukiweka akiba benki utakuwa na pa kukimbilia ukipata changamoto kwa sababu shida haipigi hodi “,alisisitiza Mangasongo.
Oscar Makwaya ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika Linda Wilaya ya Mbinga,akizungumza baada ya uzinduzi huo ameipongeza NMB kwa huduma bora za kifedha hali iliyosababisha wakulima wengi katika kijiji cha Linda kufungua akaunti kwenye Benki hiyo
Uzinduzi wa kampeni hiyo ya NMB Bonge la mpango kanda ya kusini yenye mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara umefanyika mjini Mbinga.
--
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.