BENKI ya NMB,imezindua kampeni maalum inayojulikana kwa jina la UmeBIMA yenye kuhamasisha Watanzania kukata Bima kwa ajili ya kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali ya moto,mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha mtu kupata ulemavu wa kudumu.
Meneja wa NMB kanda ya Kusini Faraja Raphael amesema,Kampeni inakwenda na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kukata Bima na itafika katika mikoa mingine ya kusini Lindi na Mtwara.
Amesisitiza kuwa,kampeni ya UmeBIMA inakwenda sambamba na kampeni kubwa ya Bima ya faraja inayalenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu.
Kwa mujibu wa Meneja huyo,gharama ya Bima ya Faraja mteja anajiunga kwa Sh.200 na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6 na inafanyika katika mikoa yote ya Tanzania na kwamba NMB inashirikiana na kampuni kumi za Bima ikiwemo kampuni ya Reliance Insurance Co Ltd
Akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Songea Faraja amesema,NMB imekuja na Bima ya Machinga ambayo itaweza kuwasaidia pale wanapopata changamoto na Bima hiyo na inapatikana kwa Sh.10,000 kwa mfanyabiashara mwenye mtaji wa Sh.laki tano na mwenye mtaji wa Sh.milioni 10 ataipata kwa Sh. 60,000.
Ametoa rai kwa wafanya biashara kuwa na Bima hiyo kwa sababu wanaweza kupoteza mali za Sh.milioni 10 kwa kutokata Bima inayopatikana kwa gharama nafuu kutoka kwenye kampuni ya Bima hapa nchini.
Amesisitiza kuwa,Bima hizo zitawasaidia wafanya biashara kuwa na uhakika na shughuli zao kwa sababu hakuna atakayesimama na hawatalazimika kuingia gharama yoyote pale watakapohitaji kuendelea na shughuli zao baada kutokea majanga.
Amesema,NMB kwa kushirikiana na kampuni inatoa Bima za magari na afya inayojulikana kwa jina la Afya Salama inayokatwa kwa Sh.laki mbili na itatumika kwa watu wanne Baba,Mama na watoto wawili na iwapo wataongezeka watu wengine muhusika ataongeza Sh.80,000 na watapata matibabu kwenye Hospitali zote hapa nchini bila kupata usumbufu.
Mwakilishi wa kampuni ya Bima ya Reliance Insurance Joel Mwakalebela amesema,kwa muda mrefu wanashirikiana na Benki ya NMB kutoa aina ya Bima mbalimbali ikiwemo Bima za magari,bima za moto na bima kwa watu Binafsi na wizi inapotokea mfanyabiashara kuibiwa mali zake.
Mwakalebela,amewataka wananchi wa mkoa wa Ruvuma kukata Bima ili kuwa na uhakika wa maisha na shughuli zao za kila siku kwani kampuni hiyo imekuja na suluhisho la changamoto zinazoweza kujitokeza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.