MFUGAJI wa Sugura wa Kisasa kutoa Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma Meshack Vila ameelezea faidi ya Nyama ya Sungura kwa afya ya binadamu.
Mfugaji huyo anapatikana katika banda la Madaba linapatikana katika viwanja vya Maonesho ya Nane nane vya John Mwakangale Mkoani Mbeya amesema Nyama ya Sungura ipo katika kundi la Nyama nyeupo ambayo kiafya ni nyama bora baada ya Samaki,Simbilisi inafuata nyama ya Sungura.
Vila amesema nyama hiyo mara baada ya kula inayeyuka mapema tumboni na inafaa kutumiwa na makundi yote ya binadamu,inaviwango vizuri vya protini na baadhi ya Madini ambayo yanasaidia katika Mwili wa binadamu katika suala zima la ukuaji.
“Kama unavyojua Mikoa yetu ya Kusini ina udumavu tunashauri watu wafuge Sungura ili watoto wapate protini waepukane na hayo matatizo”
Hata hivyo amesema ufugaji wa Sungura ni ufugaji unachochea maendeleo ya uchumi kwa haraka ambapo amesema ukianza kufuga Sungura jike wawili na dume moja unaweza kuwa na Sungura 90 hadi 100 kwa mwaka mmoja.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.