Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imeanza ujenzi wa Chuo cha ufundi stadi (VETA) , ya Wilaya ambayo inatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni mbili nukta moja (2,100,000,000) inayojengwa katika kijiji cha Linda, Kata ya Kilosa wilayani hapa ili kuwasogezea karibu huduma ya Ufundi stadi wananchi wa Wilaya ya Nyasa ili waweze kujiajiri..
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Bw. Jimson Mhagama wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake , juu ya ujenzi wa Chuo cha ufundi stadi (VETA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
Bw.Mhagama alifafanua kuwa Wilaya ya Nyasa imeanza ujenzi wa chuo cha ufundi stadi ( VETA ) inayojengwa katika kijiji cha Linda Kata ya kilosa, ujenzi ambao umeanza kwa ngazi ya msingi na kufyatua tofari, na mpaka sasa jumla ya tofari elfu thathini (30,000) tayari zimefyatuliwa.na miundombinu ya maji tayari imefika eneo la ujenzi.
Aliongeza kuwa Jumla ya majengo kumi na sita (16) ya kisasa yanatarajiwa kujengwa katika eneo la ujenzi, na Aliyataja majengo yanayaoanza kujenga kuwa ni Jengo la utawala, Jengo la Bwalo, Jiko, mabweni mawili ya wasichana na wavulana, ambayo yatakuwa na uwezo wa kulala watu mia moja na sitini (160), madarasa mawili na karakana ya uashi.
Aliongeza kutaja majengo mengine kuwa ni Karakana ya Useremala, karakana ya magari na mitambo, Karakana ya ushonaji, karakana ya Umeme, Nyumba ya mlinzi na vyoo vitatu, na nyumba ya Mkuu wa chuo.
Alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushiriki katika ujenzi wa Chuo hicho, kwa kuwa ni chuo kitakachoinufaisha jamii ya Nyasa kwa kuwa lengo la chuo, ni kuwapa ufundi Stadi wananchi wote wa Wilaya , kwa kuwa ufundi utawajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa sehemu mbalimbali.
Pia alimshukuru Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuleta fedha katika Halmashauri ya Nyasa na kuahidi atasimamia vizuri ujenzi huo.
“Natoa wito kwa Wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushiriki kikamilifu shughuli za ujenzi wa chuo hiki ambacho kitakuwa ni tiba ya ukosefu wa ajira kwa kuwa ukishapata ufundi huitaji kuajiriwa bali utajiajiri.pia namshukura sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa kutuletea fedha za ujenzi wa chuo hiki cha Ufundi stadi Nyasa kwa kuwa ametatua kero ya wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata chuo cha ufundi Songea”
Hapo awali Wilaya ya Nyasa ilikuwa haina Chuo cha ufundi stadi (VETA)ya Wilaya hivyo ilikuwa inawalazimu wananchi kutembea umbali wa kilometa 163 kwenda Chuo cha ufundi stadi (VETA) Songea, kupata huduma za Ufundi kwa kuwa hapa Nyasa kulikuwa Hakuna Chuo cha Serikali cha ufundi stadi (VETA).
Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya, amemshukuru mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa Chuo cha ufundi stadi (VETA), na kusema amewajali wananchi wa Nyasa na hivyo kuwaondolea kero ya kupata Huduma za Ufundi Stadi ( VETA) mbali na nyasa hivyo aliahidi kusimamia vizuri ujenzi huu na kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuwaondolea kero wananchi wanaotembea umbali wa kilometa 173 kufuata huduma hizo kati chuo cha ufundi stadi (VETA) Songea na kuongeza msongamano wa hali ya juu katika Chuo cha ufundi stadi (VETA)hiyo.
“Namshukuru sana mheshimiwa Rais Magufuli, kwa kunipa fedha za ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (VETA), ambayo itawasaidia wananchi wangu kwa kuwa walikuwa wakiteseka wakisafiri takribani kilometa 173 katika wilaya ya Songea, kutafuta chuo cha ufundi stadi (VETA) .Kwa sasa hakutakuwa na usumbufu , hasa vijana ambao mara baada ya kukamilika chuo cha ufundi stadi (VETA) itawaondolea usumbufu huo”.
Pia alimshukuru mh. Rais Magufuli kwa kumpa Miradi ambayo ina lengo la kutatua kero zilizokuwa zinawakabili wananchi wa Wilaya ya Nyasa.na kuitaja miradi hiyo kuwa na Ujenzi wa barabara ya Lami ya kutuka Mbinga-Mbambabay, Ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya Wilaya,Ujenzi wa VETA na miradi mingine ya Elimu.
IMETOLEWA NA
NETHO C. SICHALI
KAIMU AFISA HABARI NYASA DC.0767417597
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.