Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imeungana na watumishi pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya wilaya kama sehemu ya shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza baada ya kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru, Ndg. Milongo Sanga, amesema ameagiza zoezi hili la usafi liwe endelevu katika kudumisha hali ya usafi katika Wilaya ya Tunduru.
“Niwashukuru kwa kujitokeza katika zoezi hili la kufanya usafi, tulifanye kama jadi yetu ili kudumisha usafi katika mazingira yetu’’,.alisema Sanga.
Katika Mkesha wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, Aprili 25,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, atahutubia taifa kuelekea miaka 60 ya Muungano Tanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru amesema wananchi watashuhudia hotuba hiyo mubashara katika Viwanja vya Baraza la Idd kuanzia saa tatu usiku. ambapo, kutakuwa na maonesho ya wazi ya Televisheni kwa wananchi wote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.