• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

PEMBEJEO zisizo na ubora Tunduru zatafutiwa dawa

Imewekwa kuanzia tarehe: March 7th, 2023

KILIO cha wakulima wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, kuuziwa pembejeo na viuatilifu visivyokuwa na ubora vilivyosababisha kushuka kwa uzalishaji na kushusha ari,kimefika mwisho wake baada ya Kampuni ya Bens Agro-Star Co Ltd kusambaza kwa wingi mbolea mpya ya asilia ya samadi ya Fomi.

Mbolea hiyo inayozalishwa hapa nchini,inatajwa ni mkombozi mkubwa wa wakulima kutokana na uwezo wa kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara ikiwamo zao maarufu la mpunga na mahindi yanayolimwa wilayani humo.

Akizungumza na  wakulima wa kijiji cha Msinjili kata ya Mlingoni Magharibi wilayani humo katika shamba darasa ambalo limelimwa na kutumia mbolea  ya  Fomi,Meneja wa kampuni ya Bens AgroStar Ltd kanda ya Kusini Israel Mwampondele,amewataka wakulima  kutumia mbolea hiyo ili waweze kuvuna mazao mengi kwenye msimu mmoja.

Amesema kuwa, kwa muda mrefu wakulima wanapoteza nguvu nyingi na muda mwingi kulima kilimo kisichokuwa na tija kwa kutofuata kanuni za kilimo bora na kutotumia mbolea za kupandia na kukuzia zinazofaa kwenye shughuli zao za kilimo.

Ameeleza kuwa,wananchi wengi wanapenda kulima,lakini changamoto kubwa bado hawazingatii  taratibu na kanuni za kilimo bora,hivyo kupitia Kampuni ya Bens watahakikisha wanatoa elimu kwa wakulima kuhusu faida ya mbolea ya Fomi otesha na Fomi kukuzia.

Amesema,lengo la kampuni hiyo kuanza shughuli zake katika wilaya ya Tunduru na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla, ni kuwabadilisha wakulima kifikra kutoka kilimo cha mazoea hadi kufikia kulima kilimo cha kisasa na chenye tija na kutumia mbolea ya asili  ya Fomi.

Dkt Mwampondele,amewataka wakulima mkoani Ruvuma kuanza kutumia mbolea  ya Fomi ambayo kwa sasa ndiyo imekuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuzalishaji mazao mengi tofauti na ilivyo kuwa miaka ya nyuma.

Aliongeza kuwa,mkulima akitumia mbolea ya Fomi  na kuzingatia kanuni na taratibu za kilimo chenye tija,faida yake ni kubwa kwani katika  ekari moja ana uhakika wa kuvuna kati ya magunia 35 hadi 40.

Akielezea faida ya mbolea ya Fomi kwa wakulima wenzake Ramadhan Chalema aliyetumia mbolea hiyo kwenye zao la mahindi na mpunga alisema kuwa,hapo awali kabla hajaanza kutumia mbolea hiyo uzalishaji wa mazao ulikuwa mdogo ikilinganisha na sasa ambapo umeongezeka mara mbili zaidi.

Amewaomba wakulima wengine kuanza kutumia mbolea hiyo yenye uwezo mkubwa katika uzalishaji ili waweze kupiga hatua na hatimaye kujikwamua na umaskini kupitia shughuli zao za kilimo.

Afisa kilimo wa kata ya Sisi kwa sisi Lucy Komba alisema,wataendelea kushirikiana na kampuni ya Bens kutoa elimu ya matumizi  sahihi ya mbolea  ya Fomi ili wakulima  walime kilimo chenye tija  na wapate faida kubwa kuliko sasa.

Aidha,amewashauri wakulima wilayani Tunduru kuanza kulima na mazao mengine kama mahindi,ufuta,alizeti na soya ambayo yanasoko la uhakika ili kujiongezea kipato,badala ya kulima zao moja tu la korosho ambalo kwa sasa linakabiliwa na changamoto kubwa katika uzalishaji na soko lake.

“nawaomba sana wakulima watutumie sisi wataalam wao ili waweze kulima kilimo chenye tija na waanze kutumia mbolea hiyo ya asili katika uzalishaji mashambani”alisema Komba.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.