Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Geofrey Pinda amewahakikishia wafanyakazi wa Sekta ya aridhi mkoani Ruvuma kuwa serikali imetenga zaidi shilingi bilioni 300 kuboresha miundombinu pamoja na vitendea kazi
Hayo ameyasema hivi karibuni katika mkutano wa wafanyakazi wa sekta ya Aridhi wa mkoa Ruvuma uliofanyika Manispaa ya songea alipokutana nao na kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji pamoja na kusilikiza changamoto zinazowakabili
Pinda amesema kupitia mradi wa benki ya dunia serikali imepata Zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 300 ambazo kwa kiasi kikubwa zitakwenda kutatua adha ya vitendea kazi, hivyo Wizara itanunua magari ya kutosha pamoja na kujenga ofisi kila mkoa
“Kama nilivyoeleza tulikuwa tumetenga fedha kwenda kwenye Halmashauri ili zirekebishe ofisi za Maafisa aridhi lakini tumepata wazo kuwa tujenge ofisi zetu za wilaya kwasasababu utendaji wetu sasa unakwenda kuundiwa tume kama mamlaka zingine zinavyofanya kazi”amesema Pinda
Hata hivyo amewahimiza na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya kazi kwani itasahidia sana kuepusha migogoro mingi kwa wananchi na kuifanya wizara kustawi vizuri
Naye Kamishina wa Aridhi Msaidizi mkoani Ruvuma Idefonce Ndemela, amemweleza Naibu Waziri kwamba pamoja na kuwepo kwa changamoto lakini ofisi yake imeweka mikakati ya kuhakikisha kazi ya kisekta ya aridhi inafanyika
“Mikakati hiyo ni pamoja na kuwaomba Wakurugenzi wote kuwasilisha majina ya wadaiwa sugu wa kodi ya pango ya aridhi ili kuongeza nguvu kuwafuatilia wadeni ao pia kuhakikisha wadaiwa sugu wanapelekewa notisi za madai ya kodi mapoja na kuwafikisha mahakamani” amesema Ndemela.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.