• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS Samia alivyodhamiria kuzirejesha malikale za Ruvuma kutoka Ujerumani

Imewekwa kuanzia tarehe: February 29th, 2024

Na Albano Midelo,Songea

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Angela Kairuki amesema serikali imeanza utekelezaji wa maelekezo ya  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuandaa mpango wa majadiliano na serikali ya Ujerumani kuona namna bora ya  kurejesha malikale za Ruvuma na maeneo mengine nchini.

Hayo yamesemwa  katika hotuba ya Waziri Kairuki iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kwenye kilele cha kumbikizi ya miaka 119 ya mashujaa 67 wa vita ya Majimaji waliouawa kwa kunyongwa na wajerumani Februari 27,1906 mjini Songea.

Moja ya malikale zilizochukuliwa na wajerumani  ni kichwa cha Jemedari wa Wangoni Nduna Songea Mbano ambaye alipigwa risasi na wajerumani kisha kukata kichwa chake na Kwenda kukihifadhi nchini Ujerumani.

Baraza la Wazee wa Makumbusho ya Majimaji kwa muda mrefu wamekuwa wanaidai serikali ya Ujerumani  kuwarejeshea fuvu la Songea Mbano ambaye alionesha upinzani mkali kwa wajerumani katika harakati za kupinga ukoloni.

Waziri Kairuki amesema serikali  imekusudia kuona watanzania wananufaika na malikale zilizochukuliwa na wakoloni wa kijerumani ili watanzania waweze kunufaika na malikale hizo zilizopo nchini Ujerumani.

Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amesema historia ya harakati za ukombozi wa  Tanzania bara haiwezi kuandikwa bila kuwataja mashujaa wa vita ya Majimaji ambao walikubali kupoteza Maisha yao ili kutetea Taifa lao.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa  la Tanzania Mistica Ngongi amesema kumbukumbu za mashujaa wa vita ya Majimaji zitawezesha kizazi cha sasa na kijacho kuona na kujifunza namna babu zetu walivyoyatoa Maisha yao katika kupigania Uhuru.

Amesisitiza kuwa Vita ya Majimaji  inawakumbusha tunu za babu zetu ikiwemo ya uzalendo, ujasiri, uthubutu na umoja wao katika kutetea  maslahi ya nchi dhidi ya ukoloni.

Akizungumzia kuhusu masalia ya watu waliouawa katika Vita ya Majimaji likiwemo fuvu la Jemedari wa wangoni Nduna Songea Mbano,Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt.Frank Walter Steinmeier,akizungumza baada ya kuwafariji wahanga mjini Songea, alisema masalia hayo kutoka Afrika Mashariki yalisafirishwa hadi nchini Ujerumani na kuhifadhiwa katika makumbusho na hifadhi za kiatropolojia ambako kuna maelfu ya mafuvu ya vichwa vya binadamu.

Alisema serikali ya Ujerumani inaendelea na jitihada za kutafuta fuvu la kichwa cha shujaa Songea Mbano nchini Ujerumani ambapo ameitaja changamoto kubwa iliyopo ni kupima na kutambua  masalia halisi ya binadamu kwa fuvu la mlengwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.