• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS Samia alivyoimarisha miundombinu Mbinga vijijini ,wananchi raha tupu

Imewekwa kuanzia tarehe: March 7th, 2023

WAKALA wa barabara za vijijini na mijini Tanzania(TARURA) umesema,ujenzi wa daraja katika mto Makomba  kata ya Langiro wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limekamilika kwa asilimia 100.

Meneja wa TARURA wilaya ya Mbinga Oscar Mussa ambapo ameeleza kuwa,daraja hilo limegharimu shilingi milioni 95 na sasa lipo kwenye muda wa matazamio ya mwaka mmoja unaomalizika mwezi Machi mwaka huu.

Mussa alisema,kukamilika kwa daraja hilo linalounganisha vijiji vinne vya Mkoha na Mkoha Asili kwa upande mmoja na kijiji cha Langiro na Langiro-Asili kunatoa fursa kwa wananchi wa maeneo hayo kusafirisha mazao hasa zao maarufu la kahawa linalozalishwa kwa wingi  katika vijiji hivyo.

Alisema,daraja hil ni muhimu sana kwa kuwa,wananchi wa kata ya Langiro wanategemea kupata huduma za afya na huduma nyingine za kijamii kata jirani ya Maguu,kwa hiyo litawasaidia wananchi kupata huduma hizo kwa wakati.

Aidha alisema,kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Tarura inatarajia kujenga daraja lingine lenye urefu wa mita 10 katika kijiji cha Mkoha asili mpakani mwa wilaya ya Mbinga na Nyasa ikiwa ni mwendelezo wa mpango wake wa kuunganisha maeneo mbalimbali hapa nchini kwa barabara.

Amewataka wananchi kuwa na uchungu wa kodi zao,kwa kutunza na kulinda  barabara na kutofanya shughuli zozote kando kando ya barabara zinazoendelea kujengwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na zitumike kama chachu ya kuwaletea maendeleo yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita,kwa kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiunganishi muhimu kwa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Mbinga.

John Komba mkazi wa kijiji cha Mkoha alisema,walikuwa wakiteseka sana wanapohitaji kusafirisha mazao na bidhaa nyingine na hata wanapotaka  kufuata huduma za kijamii zikiwemo za afya  zinazopatikana kijiji jirani cha Maguu na katika kituo cha Afya Mapera.

Alisema,walikuwa  na maisha magumu zaidi hasa wakati wa masika kwani wananchi waliotaka kwenda upande wa pili kutoka kijiji cha Mkoha na Mkoha asili walilazimika kusubiri kati ya masaa manne hadi sita ili maji ya mto huo yapungue.

Alisema,hali hiyo ilisababisha kupoteza muda mwingi ambao wangeweza kutumia katika shughuli  zao za uzalishaji mali na maendeleo kwa ujumla.

Mkazi wa kijiji cha Langiro Martin Kapinga alisema,kabla ya kujengwa kwa daraja hilo,mto Makomba ulikuwa kikwazo kikubwa kwao kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita.

Kapinga,amewapongeza wataalam wa Tarura kwa kusimamia mradi huo na kuishukuru serikali ya awamu ya sita  kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa wananchi wa wilaya ya Mbinga.

Joseph Kinunda mkazi wa kijiji cha Mkoha alisema kabla ya kujengwa kwa daraja,walikuwa kwenye mateso makubwa pindi wanapohitaji kuvuka kwenda maeneo mengine na kueleza kuwa, baadhi ya wananchi wenzao wamepoteza maisha kwa kusombwa na maji walipojaribu kuvuka katika mto huo.“sisi wananchi wa maeneo haya tunaishukuru sana serikali yetu inayoongozwa na Rais  Dkt Samia Hassan,kwani katika kipindi cha miaka miwili cha uongozi wake tumeshuhudia mambo mengi mazuri yanafanyika ikiwamo ujenzi wa daraja hili”alisema Kinunda.

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.