Shule ya Sekondari ya Mpitimbi, wilayani Songea, mkoani Ruvuma, imepata maboresho makubwa baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu yake.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Patrick Matembo, fedha hizo zilitolewa katika awamu mbili.
Amesema Awamu ya kwanza (ya uboreshaji ilifanyika mwaka wa fedha wa 2023-2024 na ilihusisha shilingi milioni 751.8 zilizotumika kujenga madarasa tisa, mabweni manne na vyoo 14.
Amesema Mwaka huu, shule hiyo ilipokea shilingi milioni 128 kwa ajili ya ujenzi wa bweni lingine.
Mkuu huyo wa shule amesema Katika awamu ya pili, shule hiyo ilipokea shilingi milioni 452 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 17 na vyoo 25 na kwamba mwaka wa fedha 2024/2025, shule hiyo ilipokea shilingi milioni 25 kwa ajili ya ukarabati wa bweni la shule.
“Kwa ujumla, shule hii imepokea shilingi bilioni 1.35 tangu Dkt. Samia aingie madarakani.””,alisema.
Mwanafunzi Catherin Gama wa kidato cha sita (taasusi ya HGL) ameishukuru serikali kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Naye Faraja Lasto Jackson, mwanafunzi wa mchepuo wa uchumi, amepongeza juhudi hizo, akisema miundombinu hiyo inawasaidia wanafunzi hata baada ya masomo, hasa kupitia miradi ya shule kama kilimo cha mahindi, viazi na ndizi.
Sekondari ya Mpitimbi iliyoanzishwa mwaka 1993 ina zaidi ya wanafunzi 900 wanaosoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.