Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kuwekeza katika miundombinu ya shule.
Katika mwendelezo wa juhudi hizo, Rais Samia ametenga zaidi ya shilingi milioni 560 kwa ajili ya ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Hanga, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma.
Ujenzi wa shule hiyo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kupunguza msongamano katika shule za sekondari zilizopo.
Mradi huu unajumuisha madarasa manane, jengo la utawala, maabara za masomo ya sayansi, maktaba ya kisasa, jengo la kompyuta, pamoja na vyoo vya wasichana na wavulana.
Mradi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa wote, hasa katika maeneo ya vijijini.
Wananchi wa Hanga na maeneo jirani wamepongeza juhudi hizi za serikali, wakisema kuwa shule hiyo mpya itasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira bora na kupunguza changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.