• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS Samia atoa trilioni sita kutekeleza miradi ya TAMISEMI

Imewekwa kuanzia tarehe: September 29th, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imetoa fedha takribani Sh. Trilioni sita tangu Mhe. Rais  Samia Suluhu Hassan aingie madaraka kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akitoa salam za Wizara kwenye mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku sita ya Rais Samia mkoani Ruvuma uliofanyika kwenye uwanja wa Majimaji  mjini Songea .

Amesema "Mhe. Rais fedha ulizotoa zimeenda kila Mkoa, Halmashauri, Tarafa, Kata, Kijiji, Kitongoji na kila mtaa na zimegusa wanawake kwa wanaume, wazee, vijana, watoto na hata walemavu."

"Hakuna kundi ambalo halijafikiwa na huduma zilizopelekwa kupitia fedha hizo ulizotoa, umegusa maisha ya watanzania, umegusa mioyo yao na umeboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi,"amesema.

Amefafanua miradi iliyotekelezwa kwa kipindi hicho kuwa ni  Hospitali za Wilaya 129 mpya zimejengwa na hospitali Kongwe 50 zimekarabatiwa, Vituo vya Afya 367 vimejengwa, majengo ya kutoa huduma za dharura (EMD) 87 zimejengwa, Majengo ya kutoa huduma za Wagonjwa mahututi 28 yamejengwa, Mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya Oksjen 21 imesimikwa, magari ya kubebea wagonjwa pamoja na usimamizi wa shughuli za Afya  523 yamenunuliwa.

"Kila Halmashauri nchini imepata gari la kubebea wagonjwa pamoja na gari la usimamizi wa shughuli za afya na hapa kwenye Mkoa wa Ruvuma wamepokea magari ya Wagonjwa kwa kila Halmashauri,"amesema

Aidha, amesema kwa upande wa elimu hadi sasa Shule mpya za Sekondari kwa Kata  458 zimejengwa, Shule za Msingi 665 zenye madarasa ya awali na vyumba vya madarasa 50,050 vimejengwa pamoja na nyumba za walimu 366 zimejengwa.

"Kwa upande wa TARURA umeongeza bajeti kutoka Sh.Bilioni 253 mpaka kufikia  Sh.Trilioni 1.3, ongezeko hili ni zaidi ya asilimia  300 na hii ni kwa sababu unataka kuona barabara za vijijini zikifunguliwa na wananchi wanasafirisha bidhaa zao kwa urahisi."

“ Mhe. Rais kupitia ongezeko hili umeweza kujenga barabara za lami maeneo ambao hayakudhaniwa kuwa na lami umepandisha hadhi barabara nyingi za vijijini na mijini na zaidi umeagiza tuongeze mtandao wa barabara za lami yenye urefu wa Kilometa 23 na kwa hapa Songea Manispaa tu barabara ya lami itajengwa yenye urefu wa Kilometa 12.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.