Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali za Krimas kwa wananchi, hasa wale waliopo kwenye makundi maalum. Zawadi hizi zimewasilishwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga,ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Sanga amesema Zawadi hizi zimeandaliwa ili kuwasaidia wananchi hawa kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa furaha na kwa njia inayofaa..
"Ni hatua ya kuonesha upendo na mshikamano wa kitaifa, hasa kwa wale wanaohitaji msaada zaidi katika jamii" Alisema Ndg. Sanga na kuongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha ustawi wa jamii na kusaidia makundi maalum, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto, na wazee.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.