Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Simon Chacha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, amekabidhi zawadi kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Ruvuma ili kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
Akikabidhi zawadi hizo ambazo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuna kila sababu ya kumshukuru Rais kwa moyo wa upendo anaouonyesha.
“Tunagawa hizi zawadi kwa ajili ya vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu katika mkoa wetu wa Ruvuma, na wao siku ya sikukuu ya pasaka wapate kufurahi kama walivyo watanzania wengine, tunayo kila sababu ya kumshukuru mheshimiwa Rais kwa moyo wake wa upendo ambao amekuwa akiuonyesha,” alisema Mhe. Chacha.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Victory Nyenza, amesema kuwa utoaji wa zawadi hizo ni muendelezo wa juhudi za Serikali za kuwajali wananchi wa makundi maalum, hususan katika nyakati muhimu za sikukuu.
Amebainisha kuwa zawadi hizo zenye thamani ya shilingi milioni 2,688,000 zimelenga kuwafikia watoto 182 kutoka wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma
Kwa upande wake, Afisa Elimu wa Elimu Maalum kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Mwalimu Rashidi Mbundara, amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwajali wananchi wa makundi maalum akisema zawadi hizo zimeleta faraja kwa watoto hao.
Zawadi hizo zimetolewa kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wenye mahitaji maalum kutoka Wilaya nne za mkoa wa Ruvuma, na kila Wilaya imepata mbuzi mmoja, mchele kilo 50, sukari kilo 25, maharage, juisi, pamoja na sabuni za usafi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.