RAIS wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba Mosi 2023.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.ujumbe wa Rais Steinmeier utajumuisha viongozi wengine wa serikali, pamoja na wawekezaji wa makampuni makubwa 12; utawasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, 30 Oktoba 30 2023 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,” imeeleza taarifa hiyo.
Akiwa nchini, Rais Steinmeier atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam, Oktoba 31, 2023. Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao watapata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea kuhusu masuala muhimu yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yao.
Marais hao watapata fursa ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara, litakalohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo mbili, lililoandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani kwa ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika Hoteli ya Hyatt Regency; ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao watapokea taarifa iliyojadiliwa na Jukwaa hilo.
“Siku ya tarehe 01 Novemba 2023, Mheshimiwa Rais Stenmeier atasafiri kwenda wilayani Songea, mkoani Ruvuma kutembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji na Shule ya Msingi ya Majimaji.
Hii ni makumbusho pekee nchini Tanzania inanayoonesha historia kubwa ya Vita ya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani,” imeeleza taarifa hiyo
Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 60
Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini. Kwa mujibu wa TIC hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.