Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Rehema Madenge, Akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amefanya ziara ya kikazi ya kukagua Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 katika Kata tatu za Chiwanda,Mtipwili na Kilosa Wilayani Nyasa.
Miradi iliyokaguliwa ni Pamoja na shule ya sekondari Lovund yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Nyasa unaogharimu shilingi milioni 118.1,ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Unberkant unaogharimu shilingi milioni 128 na ujenzi wa bweni la wavulana katika sekondari ya Limbo unaogharimu shilingi milioni 130.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Katibu Tawala huyo ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari Lovund na wadau wa Elimu wa Tanzania Project, kwa kujenga shule ya Sekondari Lovund na kuikabidhi Serikali.
Amempongeza Mratibu wa Tanzania Project Mwl Dennis Katumbi, kwa kutafuta wafadhili Nchini Norway ambao wanasaidia kuleta maendeleo wilayani hapa kwa kujenga miradi mbalimbali.
Hata hivyo Katibu Tawala huyo ameuagiza uongozi wa Halmashauri Wilaya ya Nyasa kukamilisha Miradi ambayo bado haijakamilika kwa wakati na kuzingatia viwango vinavyofanana na thamani ya fedha.
Katika hatua nyingine Madenge awaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanachangia chakula ili wanafunzi waweze kupata chakula shuleni ili kuongeza ari ya wanafunzi kujifunza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Khalid Khalif ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa ikiwemo kusimamia miradi ili iweze kukamilika kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.