Wilaya ya Nyasa ndiyo kitovu cha utalii mkoani Ruvuma ikiwa na vivutio vya aina zote vikiwemo ziwa Nyasa,fukwe za asili za kuvutia,visiwa vinavyofaa kwa uwekezaji,aina 400 za samaki wa mapango,mawe yenye maajabu likiwemo jiwe la Pomonda lililopo katika kijiji cha Liuli lenye vivutio adimu,mamba anayezungumza , bonde la ufa kwenye milima ya livingstone pamoja na vivuti vingine vingi.
Wilaya ya Nyasa pia ndiyo wilaya pekee mkoani Ruvuma yenye miundombinu bora ya barabara ya lami nzito kutoka Mbinga hadi Mbambabay ikiwa na raundiabouti ya kuvutia unapoingia mjini Mbambabay.
Mbamba baya ndiyo mji pekee mkoani Ruvuma wa kitalii ambao unavutia wageni wengi kutoka mikoa mbalimbali nchini na hata nje ya nchi.Maeneo mengi katika wilaya ya Nyasa yanafaa kwa uwekezaji hasa katika sekta ya utalii ambapo mwekezaji anaweza kujenga hoteli zenye hadhi za kitalii katika fukwe za ziwa Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.