• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC aagiza majengo yote hospitali ya Namtumbo kukamilika na kutumika

Imewekwa kuanzia tarehe: September 3rd, 2022

RC AAGIZA MAJENGO YOTE HOSPITALI YA NAMTUMBO KUKAMILIKA NA KUTUMIKA KABLA YA SEPTEMBA 30

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameuagiza uongozi wilayani Namtumbo kuhakikisha majengo yote katika hospitali ya wilaya yanakamilika na kutumika.

Kanali Thomas ametoa maagizo hayo baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo na kubaini bado kuna majengo yamekamilika lakini hayatumiki na baadhi ya majengo bado hayajakamilika.

Amewataka wataalam wanaosimamia miradi wasisubiri viongozi ndipo wafike kukagua miradi na kuongeza kuwa muda wa maneno umekwisha,  kwa kuwa wananchi wanataka huduma ya afya.

“DC nakuagiza usimamie hili jengo pesa zake zinatakiwa kwisha  kabla ya tarehe 30,Septemba mwaka huu,majengo yote yanatakiwa kukamilika na kuanza kutumika,bila hivyo madhara yake ni kwamba serikali haitatuletea tena fedha za miradi’’,alisisitiza RC Thomas.

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt.Julius Ningu amemhakikisha Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia mradi huo ili ukamilike kabla ya Septemba 30 kama alivyoagiza ili kusogeza karibu huduma ya afya kwa wananchi.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Chiriku Chilumba akitoa taarifa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa,alisema Halmashauri hiyo ni mojawapo ya Halmashauri inayotekeleza ujenzi wa hospitali kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020.

Alisema katika mwaka 2019/2020 serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi  wa majengo ya maabara,mionzi,wodi ya wanaume,wodi ya wazazi na upasuaji,

Kulingana na Mkurugenzi huyo mwaka 2020/2021,serikali ilileta fedha kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ukamilishaji,ujenzi wa njia za kupita wagonjwa na  ujenzi wa wodi ya Watoto.

Chilumba amesema mwaka 2020/2021 serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya jengo la upasuaji wanawake,jengo la bima,nyumba ya maiti na ukamilishaji wa wodi ya Watoto.

Amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi milioni 800 kwa ajili ya uendelezaji wa jengo la upasuaji katika wodi ya wanaume,wanawake na nyumba ya maiti.

“Hata hivyo Halmashauri iliomba idhini ya kujenga majengo mengine ambayo ni jengo la kliniki ya Baba na Mtoto,jengo la kliniki ya afya ya macho,kinywa,meno na jengo la mama ngojea’’,alisema .

Amezitaja hatua za ujenzi wa majengo hayo kuwa,ujenzi wa jengo la kliniki ya macho,kinywa na meno ambao upo katika hatua za upandishaji kuta,ujenzi wa kliniki ya Baba na Mtoto upo katika hatua ya kuweka boksi na ujenzi wa jengo la Mama ngojea upo katika hatua za umaliziaji.

Amesema hadi kufikia Septemba 3,Halmashauri imetumia zaidi ya shilingi milioni 198 kwenye utekelezaji miradi hiyo na kiasi kilichopo ni zaidi ya shilingi milioni 600.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ruvuma

Septemba 4,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.