MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed Mei 31,2024 amepokea taarifa ya uchunguzi wa ujenzi wa soko jipya la madini Tunduru kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Amos Lugomela.
Kanali Abbasa aliunda Tume hiyo hivi karibuni ili serikali itoe maamuzi ya uwepo wa soko moja au masoko matatu ya madini ya vito wilayani humo.
Kanali Abbas aliamua kuunda Tume maalum ya wataalam ambayo ilikwenda kufanya utafiti wa hoja zote ili majibu yatakayorudi yaweze kutoa maamuzi ya serikali juu ya uwepo wa soko moja au masoko matatu ya madini wilayani Tunduru.
Taarifa ya uchunguzi uliofanywa na Tume hiyo inatarajiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa wanahabari wiki ijayo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.