MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Balozi,Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Serikali kwa kuongeza fedha miioni 50 kwaajili ya unuuzi wa Mahindi kwa mikoa ya nyanda za juu kusini.
Hayo amesema leo ofisini kwake alipotembelewa na wajumbe wa bodi ya ushauri kutoka NFRA na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita, ikiwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuzalisha Mahindi kwa chakula na Biashara ambayo italeta ari kwa wakulima wa Mahindi kuzalisha tena kwa msimu ujao.
Mkuu wa Mkoa ameongelea utekelezaji wa ununuzi wa Mahindi kuwa unaendelea vizuri ikiwemo changamoto zilizojitokeza zimeshughulikiwa na kutatuliwa kwa haraka kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo.
Ibuge amesema matarajio yake katika ununuzi wa awamu hii utaendelea kwa makusudi ya Serikali Mkulima apate faida, na kuhakikisha ununuzi unafanyika kwenye vituo ili kuwe na uwazi ya wanaofaidika na shilingi 500 kwa kilo ni Wakulima na siyo wafanyabiashara.
“Siyo kwamba hatuwapendi wafanyabiashara,ila mfanyabiashara anauwezo wa kukusanya na kujipanga kupeleka kwenye masoko mengine ruzuku iliyotolewa na Rais kwa Mkoa wa Ruvuma imeletwa kwaajli ya kunufaisha wakulima zaidi ”.
Hata hivyo Ibuge amemwagiza Meneja wa NFRA wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Halmashauri mpaka vijijini usimamizi uendelee na changamoto zitatuliwe kwanharaka pale zinapojitokeza bila kuwa na maslahi binafsi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Novemba 8,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.