• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC IBUGE akagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji kupitia ziwa Nyasa

Imewekwa kuanzia tarehe: June 13th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefanya ziara ya pili ya kukagua  maeneo ya mipakani kwa kutembelea mpaka wa Chiwindi mwambao mwa ziwa Nyasa unaogawa Tanzania na nchi ya Msumbiji.

RC Ibuge katika ziara hiyo aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyasa.

Akizungumza na viongozi na watendaji  wa serikali katika kijiji cha Chiwindi,wilayani Nyasa,RC Ibuge ameagiza ulinzi na usalama katika eneo la mpaka kuimarishwa zaidi ili wananchi wanaoishi mpakani wasiwe na hofu bali waendelee kushiriki katika kazi za uzalishaji mali.

Hata hivyo amewataka wananchi wanaoishi mpakani kuwa walinzi wa kwanza na endapo wataona dalili za hatari wasipuuze, bali watoa taarifa haraka katika ngazi za juu ili hatua zichukuliwe haraka.

Ametoa rai kwa wananchi na wafanyabiashara wanaovuka mpaka kwenda Msumbiji kufuata maelekezo ya serikali,na hasa kutokana na kile ambacho kinaendelea katika nchi ya Msumbiji vikiwemo vitendo vya ugaidi ambapo amesisitiza kipaumbele cha kwanza kiwe ni maslahi ya Taifa.

Amewatahadharisha viongozi na watendaji waliopo mpakani wasiruhusu vitendo ambavyo vinahatarisha amani katika mipaka ya nchi  ukiwemo mpaka wa Chiwindi ambako kuna mwingiliano wa wageni kutoka Msumbiji na kuingia Tanzania.

“Mipango ya serikali ni mikubwa,Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ana lengo la kuiendeleza nchi hii ipige hatua kubwa katika maendeleo’’,alisisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo amesema bila amani na utulivu hakuna maendeleo,ambapo amewapongeza wananchi mwambao mwa ziwa kwa kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo cha zao la muhogo.

Hata hivyo amesema serikali kupitia ngazi ya wilaya ya Nyasa, inaandaa mpango   kuviwezesha vikundi vidogo ili  viweze kufanya kilimo cha ziada cha kuongeza kipato ambapo amesema wilaya ya Nyasa inafaa kwa kilimo cha michikichi ambacho kinazalisha mafuta ya kula ambayo yana soko kubwa hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa ziara hiyo,ambayo amesema imeleta faraja kubwa kwa wananchi wa kijiji cha Chiwindi kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Hii ni ziara ya pili ya RC Ibuge kukagua maeneo ya mipaka katika Mkoa wa Ruvuma,ambapo katika ziara ya kwanza RC Ibuge alikagua mpaka wa Mkenda unaoigawa Tanzania na Msumbiji kupitia Mto Ruvuma wilaya ya Songea.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 13,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.