Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewaagiza wataam wa afya kuhakikisha elimu ya chanjo Mpya ya UVIKO 19 aina ya sinopharm inatolewa kwa wananchi ili wapate uelewa kabla ya kuamua kuchanja kwa hiari.
Ametoa agizo hilo wakati anazungumza na wataalam wa afya kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma baada ya Mkoa kupokea dozi zaidi ya 31,000 za chanjo ya UVIKO aina ya sinopharm ambazo tayari zimegawiwa katika Wilaya zote.
”Nataka elimu ya chanjo hii ipewe kipaumbele kwa sababu chanjo hii ni tofauti na chanjo iliyotangulia,wananchi wa Ruvuma wana mwamko mkubwa wa kuchanja “,alisema RC Ibuge.
Kwa mujibu wa wataalam chanjo ya sinopharm inatolewa mara mbili ili kukamilisha dozi hivyo RC Ibuge amesisitiza elimu sahihi kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kurudia kuchanja siku 28 baada ya kupata chanjo ya kwanza.
Hata hivyo kulingana na wataalam wa afya mtu anayeruhusiwa kupata chanjo ya sinopharm ni mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na ambaye hajapata chanjo ya kwanza ya UVIKO aina ya JJ na kwamba chanjo zote ni salama kwa matumizi ya binadamu na zina uwezo Sawa.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 24,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.