MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewataka wadau wa kilimo cha kahawa kuendelea kushikamana ili kuongeza uzalishaji, thamani ya soko na kukuza kipato kwa wananchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa kahawa wa Mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa Manispaa ya Songea leo.
Amesema Mkoa wa Ruvuma umezalisha wastani wa tani 23,000 kwa msimu wa 2021/2022 ambayo imetoa kahawa safi tani 19,152 iliyouzwa hivyo Mkoa wa Ruvuma kwa kuzingatia malengo ya kitaifa umelenga kuzalisha kahawa kavu tani 75,000 itakayotoa kahawa safi tani 60,000 ifikapo mwaka 2025.
‘’Ndugu wadau wa kahawa ili kuhakikisha bei ya kahawa inaongezeka kila mmoja anawajibu wa kufanikisha uimarishaji wa ubora wa zao kwa kadri ya kila mmoja atakavyopaswa kutimiza wajibu wake’’ amesisitiza RC Ibuge.
Hata hivyo RC Ibuge amesema licha ya jitihada za dhati zinazofanywa na wadau wote za kuongeza uzalishaji, bado unywaji wa kahawa upo chini kwa wastani wa asilimia 7 hadi 10 hivyo amewasihi wadau kujijengea mazoea ya kunywa kahawa kwa manufaa ya kiafya.
Kwa upande wake mjumbe wa Bodi ya kahawa ambae amemwakilisha Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa ndugu Gotam Haule amewapongeza wadau wote kwa juhudi kubwa za pamoja wanazozifanya ili kuhakikisha zao hilo linazalishwa kwa wingi.
Mkoa wa Ruvuma umeshika nafasi ya pili kitaifa kwa uzalishaji wa zao zao la kahawa.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni na Jackson Mbano
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mei 30 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.