Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema ameweka jiwe la msingi katika jengo jipya la upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph Peramiho Songea.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dr Ansgar Stuffe OSB amesema fedha ambazo zinatumika kutekeleza mradi huo zimetolewa na Msamaria Mwema ambaye aliandika wosia kabla ya kufariki kwamba shilingi bilioni 1.2 zitumike kuongeza miundombinu mipya katika hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph Peramiho.
Dr Ansgar amesema mara baada ya kukamilika jengo hilo huduma mbalimbali za upasuaji zitakuwa zinatolewa katika hospitali hiyo badala ya wananchi kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.