MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza katika kikao kazi hicho kilichohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamati ya ulinzi ya usalama ,pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali ya Mkoa amesema lengo ni kujua miradi inayotekelezwa mkoani hapo ilipofikia.
“Nimepokea taarifa kutoka idara mbalimbali naomba viongozi kuwa wamoja na kujadili changamoto zilizopo na kuzitatua kwasababu wote tunajenga nyumba moja”.
Ibuge amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia miradi yote, ikiwemo vituo vya afya kutoa huduma bora pamoja na miradi ya Elimu inayojengwa kumalikika kwa wakati.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Mei 27,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.