• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC MNDEME afungua maonesho ya nanenane ngazi ya Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 5th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefanya ufunguzi wa maonesho ya nanenane ngazi ya Mkoa kwa kueleza mafanikio makubwa ambayo yamepatikana ikiwemo uzalishaji wa chakula cha kutosha hali ambayo imefanya Mkoa kuwa na ziada ya chakula tani 877,000.

Katika hotuba ya Mndeme ambayo ilisomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Nsenye kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,amesema  kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula Mkoa umepangiwa na serikali kununua zao la mahindi kiasi cha tani 70,000 kwa shilingi 550 kwa kilo kupitia Wakala wa Usalama wa Chakula wa Taifa(NFRA).

Hata hivyo Mndeme amesema Mkoa unatambua changamoto ya soko kwenye zao la mahindi na unaendelea na jitihada za kuwatafutia wawekezaji watakaosaidia katika usindikaji na kuongeza upatikanaji wa soko.

“Mkoa wa  Ruvuma kwa mwaka 2015 ulikuwa na  jumla ya ng’ombe 117,374,mbuzi 227,186,nguruwe 223,976,ambapo mwaka 2020 mifugo imeongezeka na kufanya Mkoa kuwa na ng’ombe 190,514,mbuzi 272,147,kondoo 30,625 na nguruwe 315,923’’,alisema Mndeme.

Amesema ongezeko la mifugo limesababisha kuongezeka kwa mazao ya mifugo na kufikia tani 7,851.58 za nyama ya ng’ombe,tani 4,906.65 za nyama ya mbuzi,tani 871.2 za nyama ya kondoo,tani 14,033.32 za nyama ya nguruwe na tani 179,345.

Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni  tatu kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa iliyopo Manispaa ya Songea yenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 100 na mbuzi 200 kwa siku ambapo amesema hiyo ni fursa kwa wafugaji.

Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Onesmo Ngao amesema viwanja vya maonesho ya nanenane ngazi ya Mkoa vilivyopo  Msamala Manispaa ya Songea ambavyo vinamilikiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, bado havijakamilika, hivyo ametoa rai kwa wadau kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanashiriki kukamilisha  viwanja hivyo.

Viwanja hivyo vikikamilika kwa asilimia 100,watazamaji wengi wataingia kwa kuchangia na uwanja utaweza kujiendesha wenyewe na kupungua mzigo wa wadau kuendelea kuchangia.

Kaulimbiu ya mwaka huu ya maonesho ya nanenane inasema ‘’kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi chagua viongozi bora 2020’’,kaulimbiu hii imelenga kuwasisitiza wananchi wote  kushiriki katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 5,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.