Mkoa wa Ruvuma umeendelea kutekeleza kwa mafanikio Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa kuhakikisha kuwa Serikali katika ngazi zake zote – Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaendelea na jitihada za kuzikabili changamoto mbalimbali ikiwemo kuondoa umasikini, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali za umma, kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya raia na mali zao. Katika kipindi cha taarifa hii, Mkoa umepiga hatua za kimaendeleo katika sekta za kilimo, mifugo, ushirika, uvuvi, madini, maliasili, miundombinu, mawasiliano na uchukuzi, nishati, afya, elimu na maji. Aidha, kumekuwa na mafanikio katika Sekta ya maendeleo ya jamii na utawala bora, kama inavyoonekana kwenye maelezo yafuatayo kwa kina katika sekta zote.
SEKTA YA ELIMU
Idadi ya Shule; Tangu mwaka 2015 hadi 2020 Mkoa umekuwa na ongezeko la idadi ya shule za msingi 103 kutoka idadi ya shule 670 zilizokuwepo mwaka 2015 hadi shule 773 mwaka 2020. Shule za sekondari zimeongezeka kutoka idadi ya shule 111 mwaka 2015 hadi shule 205 kufikia mwaka 2020 sawa na asilimia 54 ambalo ni ongezeko la shule 94.
Uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka na kuimarika ambapo kuna ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa idadi ya wanafunzi 50021 hadi kufikia Juni 2020 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi 47978 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilmia 4.2 .
Itaendelea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.