• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC MNDEME awapongeza Tunduru kwa kupata hati safi mara tano mfululizo

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewapongeza  madiwani,wabunge na watalaam wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kupata Hati safi kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya Hesabu za mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2019.

Mndeme ametoa pongezi hizo wakati anafungua kikao maalum cha Baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu hoja na mapendekezo ya Hesabu za TAMISEMI kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 mjini Tunduru.

“kitendo cha kupata hati safi ni  matokeo ya utendaji kazi mzuri wenye mshikamano na ushirikiano kati ya watalaam wa Halmashauri na madiwani,hii ni kutokana na Halmashauri kuundwa na pande mbili,inapotekea mnafanya vizuri,hata sisi viongozi katika ngazi ya Mkoa tunafarijika sana hongereni sana’’,alisema Mndeme.

Hii ni mara ya tano mfululizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kupata hati safi kuanzia mwaka wa fedha wa 2014/2015 hadi 2018/2019 ambapo Mndeme amesisitiza kuwa kupata hati safi mfululizo iwe chachu ya kufanya vizuri zaidi.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki kuhakikisha miradi yote ya maendeleo katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma inakaguliwa na kufanyiwa tathimini.

 “Iwapo kuna uzembe uliosababisha  miradi kutotekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa nipate taarifa ya hatua stahiki zilizochukuliwa kwa watumishi wazembe kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba,2020’’,alisisitiza Mndeme.

Mndeme pia ameagiza kupata sababu ambazo zimekuwa zinasababisha hoja za aina moja kujitokeza mara kwa mara  na hoja ambazo hazijafungwa ambapo ameagiza kupata orodha ya majina ya watumishi husika na vyeo vyao na hatua walizochukuliwa kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Mei 23,2020

Tunduru

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.