MKUU WA MKOA RUVUMA AZUIA LIKIZO ZA WATENDAJI WAKUU WA MKOA NA WILAYA
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kuhakikisha mkoa wake unawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 wanapata nafasi ya kusoma kwenye madarasa ya kutosha,amesitisha likizo zote za watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari.
Mndeme ametoa agizo hilo jana wakati wa kikao chake na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vyumba vipya 142 vikamilike kujengwa
Viongozi walizuiwa likizo ni Katibu Tawala Mkoa,Wakuu wote wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri ,Afisa Elimu Mkoa na wale wa wilaya zote pia wahandisi wa ujenzi wa halmashauri.
“Nataka katika halmashauri zote zenye upungufu wa vyumba madarasa hakuna kiongozi kwenda likizo ya mwisho wa mwaka hadi madarasa mapya yakamilike kujengwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 waingie darasani ” alisema Mndeme
Awali akitoa taarifa fupi ya hali ya hali ya miundombinu ya madarasa Katibu Tawala Mkoa Prof Riziki Shemdoe alisema jumla ya wanafunzi wapya 1,556 watahitaji madarasa mapya ya kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari .
Prof.Shemdoe amezitaja halmashauri zenye upungufu wa madarasa na idadi kwenye mabano kuwa Tunduru(35),Mbinga (18),Songea (09),Songea Manispaa (09),Namtumbo (26)
Halmashauri zingine zenye upungufu ni Nyasa (32),Mbinga Mji (09) na Madaba (04)
Aidha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mndeme amezuia safari za mafunzo za madiwani wote katika halmashauri nane za Ruvuma hadi watoto wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hapo mwakani watakapoingia darasani..
Mwisho
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.