• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC MNDEME; Mkoa wa Ruvuma una ziada ya chakula tani 877,048

Imewekwa kuanzia tarehe: August 5th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma  Christina Mndeme amesema Mkoa wa Ruvuma una ziada ya chakula  tani 877,048 na kwamba  Mahitaji ya chakula katika Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2020 ni tani 469,172 ikilinganishwa na uzalishaji wa mazao ya chakula ni tani 1,346,220.

Mndeme alikuwa anazungumza kwenye Mkutano wa  14 wa Baraza la wafanyakazi wa TANROADS  kitaifa ambao umefanyika kwa siku mbili  mjini Songea mkoani Ruvuma kwenye ukumbi wa Parokia ya kanisa katoliki la Bombambili na kufunguliwa na  mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele.

Akizungumza kwenye mkutano huo ulioshirikisha wajumbe 103 kutoka mikoa yote nchini,Mndeme  amesema Mkoa wa Ruvuma umeshika nafasi ya kwanza katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini katika msimu wa kilimo  2018/2019,ambapo amewataka wajumbe wa mkutano huo wakiwa Ruvuma wale kwa sababu Mkoa una chakula cha kutosha ukiwemo ugali,wali,maharage na samaki watamu kutoka ziwa Nyasa.

Amezitaja Takwimu za uzalishaji wa mahindi mkoani Ruvuma  katika msimu wa mwaka 2015/2016 zinaonesha Mkoa wa Ruvuma ulilima Hekta 231,936.6 zilizotoa mavuno ya Tani 736,692.8 na katika msimu wa mwaka 2019/2020 Mkoa wa Ruvuma ulilima hekta 268,008 zilizotoa mavuno ya Tani 787,321 hii ni sawa na ongezeko la Tani 50,628.

Mndeme amesema Mafanikio hayo yametokana na uwepo wa nguvu kazi ya kutosha na utayari wa wananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji ambapo hadi sasa Mkoa una  chakula cha kutosha na ziada.

“Mkoa una jumla ya hekta 4,007,746 za ardhi zinazofaa kwa kilimo, katika kipindi cha Miaka mitano kuanzia mwaka 2015 - 2020 Mkoa umeweza kuzalisha tani 8,547,816 za mazao hadi kufikia mwaka 2020’’,alisisitiza.

Hata hivyo Mndeme ameyataja Mahitaji ya chakula katika Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2020 ni tani 469,172 ikilinganishwa na uzalishaji wa mazao ya chakula ni tani 1,346,220 na hivyo Mkoa una ziada ya chakula tani 877,048.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amemshukuru Rais wa Dkt John Magufuli kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kazi kubwa ambayo ameifanya ya kuboresha miundombinu ya barabara,,uwanja wa ndege wa Songea na miundombinu ya bandari katika ziwa Nyasa hali ambayo imeufanya Mkoa kupatikana barabarani,majini na angani.

Amesema miundombinu hiyo imetekelezwa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano na kwamba TANROADS ndiyo wadau wakuu katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba hivi sasa mtandao wa barabara kuunganisha Mkoa mzima wa Ruvuma unaendelea ambapo hivi sasa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami  yenye urefu wa kilometa 67 kwa gharama ya shilingi bilioni 129 kutoka Mbinga kwenda Nyasa umefikia zaidi ya asilimia 52.

Kuhusu ujenzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Songea,Mndeme amesema hivi karibuni ndege aina ya bombadier zitaanza kutua katika uwanja huo ambao serikali imetoa shilingi bilioni 37 kukarabati na kuongeza urefu na kwamba mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya CHICCO ya nchini China upo katika hatua za mwisho hali ambayo itawezesha kurejesha tena safari za ndege ya bombadier mkoani Ruvuma,baada ya kusitishwa ili kupitisha ujenzi na ukarabati wa uwanja huo.

"Ruvuma ya sasa imefunguka sio sawa na Ruvuma ya zamani,nakupongeza sana Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano kwa kusimamia miradi ya ujenzi ambayo inakwenda vizuri,serikali imetoa mabilioni ya fedha kukamilisha ujenzi wa barabara ya lami ya Mangaka mkoani Mtwara hadi Songea  hali ambayo imeunganisha mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma kwa kuwa na mtandao wa lami'',alisema Mndeme.

Akizungumza kabla ya kufungua mkutano huo mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Wizara yake imejitahidi kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imechangia kuliingiza Taifa la Tanzania katika uchumi wa kati kutokana na ujenzi wa miundumbinu mbalimbali  ya barabara,majini ya angani ikiwemo ununuzi wa ndege.

Mhandisi Kamwelwe amesema serikali ya awamu ya tano imejitahidi kutekeleza miradi mbalimbali kama ilivyo katika Ilani ya CCM ambapo mawasiliano kwa nchi nzima imefikia asilimia zaidi ya 90 na kwamba utekelezaji katika nishati ya umeme vimebakia vijiji 3000 tu kutekeleza katika nchi nzima na kwamba hivi sasa wananchi wanafurahi kuishi katika nchi yenye maendeleo makubwa na kwamba hivi sasa kuna dalili za vijiji kufutika kwa sababu kila kijiji kinaonekana ni mji mdogo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Agosti 4,2020


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.