Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuhakikisha ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa vyenye thamani ya shilingi milioni 200 vinakamilika Novemba 30 kama ilivyopangwa.
Kanali Thomas ametoa agizo hilo baada ya kukagua mradi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari Magagura na vyumba viwili katika sekondari ya Mpitimbi vilivyogharimu shilingi milioni 100.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Katika Wilaya ya Songea pekee serikali imetoa shilingi bilioni 1.9 kujenga madarasa 96.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Katika Mkoa wa Ruvuma imetoa shilingi bilioni 3.2 kujenga madarasa 156 katika shule za sekondari.
Kukamilika kwa madarasa hayo kutapunguza uhaba wa madarasa katika shule za sekondari.
Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.