MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuangalia upya masharti yanayokwamisha wananchi kuboresha majengo yao, ili kutoa fursa ya maendeleo ya mji na kuinua uchumi wa wananchi.
Amesema ni muhimu kuruhusu maboresho ya majengo kwa kufuata taratibu za mipango miji badala ya kuwazuia wananchi bila sababu za msingi.
Kanali Ahmed ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Manispaa ya Songea, ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akiwa katika Kituo cha Afya Mjimwema, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Duka la Dawa, ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.
Katika hatua nyingine ya ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ametembelea mradi wa ujenzi wa maegesho ya malori katika Kata ya Lilambo, mtaa wa Lilambo A.
Ametoa wito kwa Halmashauri kuhakikisha miradi yote inasimamiwa kwa viwango bora na kukamilika kwa wakati, ili kuleta tija kwa jamii na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.