Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amefungua kikao Cha ukusanyaji wa maoni ya uandaaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ngazi ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Akifungua kikao hiko MKuu wa Mkoa amebainisha kukaribia ukomo kwa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 ambayo imetekelezwa kuanzia mwaka 2000 na kueleza juhudi za Serikali za kuandaa Dira mpya ya Maendeleo ya mwaka 2025- 2050 itakayotumika kwa miaka 25 ijayo.
"Katika hatua hizi za mwanzo Jukumu la kuandaa limekabidhiwa kwa timu kuu ya kitaalam ya Dira ,na Moja ya kazi muhimu ni kushirikisha Watanzania wengi kadri iwezekanavyo katika kupata maoni kuhusu mtanzania, jamii na Tanzania waitakayo ifikapo miaka hiyo ya 2050" ameeleza Mkuu wa Mkoa
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo ameitaja Dira ya Taifa ya ya mwaka 2025 imeundwa na nguzo kuu tano ambazo ni maisha Bora na mazuri, kuwepo kwa mazingira ya amani,usalama na umoja, utawala na uongozi Bora, ujenzi wa jamii iliyoelimika na kupenda kujifunza na kujenga uchumi imara.
Makondo ameyataja mafanikio ya utekelezaji wa Dira ya 2025 ikiwemo kuwezesha nchi kupata mafanikio ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kama vile nchi kuingia katika kundi la kipato cha kati cha chini, kuimarika kwa huduma ya elimu na afya na kuimarika kwa huduma za barabara na miundombinu
Kwa upande wake Katibu wa CCT Mkoa wa Ruvuma, Fulko Hyera ameishukuru Serikali kwa kwa kutekeleza mipango iliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 katika sekta mbalimbali akishauri uboreshwaji zaidi katika sekta ya Elimu na Afya ili kuimarisha zaidi shughuli za uzalishaji mali na uchumi kwa Dira ya mwaka 2050
Mchakato wa maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ulizinduliwa na Makamu wa Rais Dkt. Isdor Mpango jijini Dodoma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.