Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amekagua mradi wa mabasi wa Kijiji cha Parangu, Halmashauri ya Wilaya ya Songea .
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Kanali Abbas amemuagiza mkandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo.
Amesisitiza ubora wa kazi na kuwapongeza wananchi wa Parangu kwa kushiriki katika ujenzi wa stendi kwa kuchimba msingi, mashimo ya vyoo, kusafisha eneo, kumwagilia maji, na kusongeza vifaa.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Parangu, Bw. Cosmas Mbute, akiwasilisha taarifa ya mradi huo, amesema kuwa ujenzi wa stendi ya mabasi ulianza tarehe 17 Desemba 2022 baada ya kupokea fedha za awamu ya kwanza kiasi cha Tsh. 202,833,871.43.
Amesema hadi Kufikia Mei 2023, waliomba fedha za awamu ya pili kutoka TASAF kiasi cha Tsh. 136,000,000 ambapo hadi sasa zimetumika zaidi ya shilingi milioni 315.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.