• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA akemea mila potofu zinazokandamiza wanawake

Imewekwa kuanzia tarehe: March 9th, 2023

MKUU  wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekemea mila potofu kwa baadhi ya jamii zinazoendelea kuwakandamiza wanawake na kuwapoka mizania ya haki na usawa.

Kanali Thomas amesema hayo wakati anazungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika  katika viwanja vya Bandari mjini Mbambabay wilayani Nyasa.

Amesema vitendo hivyo vinaendelea kusababisha  kuwepo kwa lindi la umasikini katika ngazi ya kaya kwa miongo mingi hali inayoathiri malezi na makuzi ya Watoto katika jamii.

Ameongeza kuwa wanawake wengi wananyimwa haki hasa katika umiliki wa rasilimali ardhi,kukosa dhamana za kuwezesha umiliki wa rasilimali ardhi,kukosa dhamana ya upatikanaji  wa huduma za kifedha,haki ya kupata elimu na haki ya kuchaguliwa kuwa kiongozi katika ngazi ya jamii.

“Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imesimama kidete katika kulinda haki na kujenga usawa kwa jamii yote,serikali inahakikisha wanawake wanapata haki na kuwa majasiri katika kujiamini na kujitokeza kugombea na kushinda nafasi mbalimbali za uongozi’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Ametoa rai kwa wanawake kutoa taarifa kwa wakati inapotokea unyanyasaji au ukatili wa aina yoyote sanjari na kutoa ushirikiano katika kutoa elimu ya kupinga ukatili na unyanyasaji.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wanawake inayotokana na asilimia kumi ya mapato,ambapo amesema katika Mkoa wa Ruvuma zaidi ya shilingi milioni 588 zimetolewa kwa wanawake katika kipindi cha mwaka 2022/2023.

Awali Risala ya wanawake wa Mkoa wa Ruvuma iliyosomwa na Mariam Juma kwenye maadhimisho hayo  imezitaja changamoto zinazoendelea kuwakabili wanawake zikiwemo za kuwepo mfumo dume unaolindwa na mila na desturi potofu katika jamii.

Risala hiyo imezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni wanawake kukosa haki ya kumiliki ardhi,kupigwa,kubakwa,kutelekezwa na kunyang’anywa mali na ndugu wa mume pindi wanapofiwa na waume zao na kunyimwa haki zao za msingi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho  ameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya CCM yam waka 2025 ambayo amesema imetelezwa kwa kiwango kikubwa baada ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuleta fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma.

Komredi Mwisho pia amempongeza Rais Dkt Samia kwa kuimarisha demokrasia siku ya wanawake duniani ambapo ameungana na wanawake cha CHADEMA kama mgeni rasmi.

Kaulimbiu ya siku ya wanawake Duniani ya mwaka huu inasema Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia;chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.