Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ametunukiwa nishani nne na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hafla hiyo imefanyika leo mkoani Ruvuma mbele ya maafisa wa jeshi na askari wa Kanda ya Kusini, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango mkubwa wa Kanali Ahmed katika utumishi wa umma na kuimarisha usalama wa mkoa huo.
Akizungumza baada ya kupokea nishani hizo, Kanali Ahmed ameonesha furaha na kueleza kuwa ni heshima kubwa kwake kutambuliwa kwa juhudi zake. Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini kazi yake na kumpa fursa ya kuendelea kulitumikia taifa.
Aidha, amemshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi pamoja na maafisa wa JWTZ waliokuwa sehemu ya tukio hilo, akisisitiza kuwa nishani hizo ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
Tukio hilo limeonesha mshikamano kati ya serikali na vyombo vya ulinzi na usalama, huku wananchi wa Ruvuma wakilipokea kwa furaha kama ishara ya uongozi bora na maendeleo endelevu ya mkoa huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.