MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed amejiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Manispaa ya Songea
Kanali Abbas ameonesha mfano mzuri wa umuhimu wa ushiriki wa viongozi katika mchakato wa uchaguzi .
Akizungumza mara baada ya kujiandikisha Kanali Abbas amehimiza wananchi kujiandikisha na kushiriki kikamilifu zoezi la uandikishwaji daftari la kupigia kura ambapo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishwaji vilivyopo kwenye maeneo yao ili waweze kuwa na sifa za kuwachagua viongozi watakao waongoza na kuwaletea maendeleo.
“Nitumie fursa hii kumshukuru na kumpongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukuza Demokrasia nchini “”, alisema.
Amewapongeza na kuwashukuru viongozi wa dini,wananchi pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya,Halmashauri na watendaji wote kwa maandalizi mazuri yaliyofanywa katika kutoa elimu kuelekea Uchaguzi wa serikali ya mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.