Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Labani Thomas amewataka Wananchi mkoa umo wajitokeze kupima afya zao na kupata ushauri wa kitaalam wa magonjwa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake RC amesema Mkoa wa Ruvuma unatarajia kupata huduma ya matibabu ambayo itaanza tarehe 8 hadi tarehe 10 mwezi November 2022 Uwanja wa MajiMaji katika Halmshauri ya Manispaa ya Songea.
Amesema matibabu hayo yatatolewa kwa ushirikiano wa madaktari bingwa kutoka Nchi ya China kwa kushirikiana na madaktari wa Manispaa na kutoka Hospitali ya Mkoa pia amewaomba Wananchi wajitokeze kupima afya zao kwani huduma ya matibabu hayo ni bure
“Kwa wale wote ambao wamejiandaa kuona hii ni kama fursa ya kunufaika kupitia wananchi wezao (Vishoka) niwaambie hiyo fursa haipo mtu hasije akatoa senti tano kwa mtu yoyote awe daktari au askali huduma ni bure mjitokeze” alisema Kanali Thomas.
Naye mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Ruvuma Mhe, Jacqueline Msongozo ametoa wito kwa wanaruvuma wote kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma pamoja na makundi mbalimbali wajitokeze kupata huduma ya matibabu ambayo yatatolewa siku tatu mkoani umo
“Wananchi mjitokeze kwa wingi kwani huduma hii ni bure haina malipo kuanzia vipimo matibabu na dawa vitatolewa bure kwahiyo changamkieni hii fursa wananchi wezangu nimatarajio yangu mtajitokeza kuanzia asubuhi katika viwanja vya majimaji”alisema Msongozo.
Hata hivyo amewataka wananchi kuwai kufikia mapema uwanjani ili waweze kujisajili mapema kwani itawasiadia kuhudumiwa kwa muda sahihi na kujua nafasi yako ya matibabu aidha unaweza kupiga simu 0753665484
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.