MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezindua Jumuiya ya watumia Maji bonde dogo la Juwaluru na Juwaluha Mkoani umo
Hafla ya uzinduzi huo umeudhuriwa na wadau wa watumia maji kutoka halmashauri ya Madaba na Namtumbo za Mkoa umo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Herittage mjini Songea.
Akizungumza katika uzinduzi huo Kanali Thomas, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake kwa kuleta maendeleo nchini kwa kuwajali wananchi wanapate maji safi na salama na asa kuhakikisha anamtua Mama ndoo kichwani
Kanali Thomas alisema Wananchi wanajukumu la kutunza vyanzo vya maji na mazingira ili kujihakikishia upatikanaji wa maji kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi katika sekta mbalimbali vile vile kwa uifadhi wa kizazi cha sasa na baadae
“Maji yanaukomo na ukomo huo unatokana na shughuli zetu za kibinadamu, zisizo zingatia taratibu kwenye vyanzo vya maji ikiwemo ukataji miti hovyo hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu analinda na kutunza vyanzo vya maji kwa maana maji ni uhai wetu na hayana mbadala” alisema Thomas.
Pia amewasisitiza Wadau kuwa wakasimamie utekelezaji wa sera na sheria, kanuni na miuongozo ya rasimali maji na mazingira pia kuendelea kutoa elimu ya uifadhi vyanzo vya maji na mazingira kwa jamii kwa kupanda miti na kufanya shughuli kutoka mita 60 kilipo chanzo maji.
Naye Mkurugenzi wa bonde la Ziwa Nyasa na Songea, Alice Englabeth ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono uifadhi wa vyanzo vya Maji kwa kutoa Fedha kupitia Wizara ya Maji zilizo wezesha kuunda jumuiya ya watumia Maji bonde ndogo la Lutukira na Ruhuhu pamoja na bonde la Lumecha na Hanga.
“Jumuiya ya watumia Maji hii ni Taasisi ambayo hipo chini kwenye ngazi ya usimamizi wa Maji ikiongozwa na Waziri wa Maji, pia bonde la Ziwa Nyasa mipaka yake haiishi ndani Nchi yetu kwahiyo tukifanya mambo chanya italeta matokeo kwa Nchi zingIne” alisema Englabeth.
Joseph Ndumba ni Katibu wa Jumuiya ya Juwaluha amesema wao kama wanajumuiya baada ya kupata elimu ya uifadhi vyanzo vya maji na mazingira watafanya mikutano kila Kijiji na kutoa elimu kwa Wananchi ili waanze kuchukua hatua ya kuvitunza vyanzo vya maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.