MKUU wa MKoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekabidhi magari manne na pikipiki 15 kwa Halmshauri ya Wilaya ya Namtumbo na Tunduru, lengo kuu ni kuendelea kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa maliasili katika mfumo wa Ikolojia kwenye Ushoroba wa Selous-Niassa katika Halmashauri hizo.
Vitendea kazi hivyo vimetolewa kupitia mradi wa Selous Ecosystem Conservation and Development (SECAD) ambao unatekelezwa kwa fedha za msaada kutoka Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani KFW
Hafla hiyo ya makabidhiano ya vitendea kazi hivyo vipya imefanyika katika viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea leo Mei 25, 2023 na imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa utalii wakiwemo WWF.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.